Mshambuliaji wa Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC toka Jamhuri ya Afrika ya kati Gervais Kago, ambaye nusura apelekee mchezo wa ngao ya jamii kati ya Simba SC na Yanga (mchezo wa watani wajadi) ameachwa katika usajili wa msimu ujao pamoja na beki toka Uganda Ferick Walulya.
Uongozi wa Simba walitishia kugomea mchezo huo kushnikiza usajili wake uliotumia mfumo ambao TFF wameuacha kuutumia upitishwe na aweze kutumiwa katika mchezo huo wa Ngao ya jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alisema klabu yake haina mpango na wachezaji Ferick Walulya wa Uganda na Gervais Kago wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Alisema wachezaji hao mikataba yao imeisha, hivyo Simba haitahitaji kuwaongezea na kwamba watakuwa huru kujiunga na timu nyingine.
Akizungumzia vipaumbele katika usajili wa mwaka huu, alisema ina mkakati wa kuboresha zaidi usajili katika safu ya beki wa kati. Pia alisema wanahitaji kupata mrithi wa kiungo mahiri wa timu hiyo aliyefariki hivi karibuni kwa ajali ya gari, Patrick Mafisango.
Aliongeza kuwa klabu yake imejipanga kuhakikisha kuwa usajili wa mwaka huu unafanyika kiumakini zaidi huku akisisitiza kuwa nguvu pia itawekwa katika kuwasajili wachezaji wa kikosi cha vijana cha timu hiyo.
No comments:
Post a Comment