tuwasiliane

Tuesday, May 29, 2012

29 May. HALI TETE UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA RUAHA



vurugu kubwa ziliibuka jana, katika kata ya ruaha, katika wilaya ya kilosa baada ya kushindikana kufanyika kwa uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji wa kata hiyo siku ya jumapili ya tarehe 27/05/2012.uchaguzi huo ulikuwa ufanyike baada ya kufukuzwa mwenyekiti wa kijiji hicho baada ya kugundulika kuwa ni mbadilifu.ina daiwa kuwa zoezi la kujiandikisha wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi huo lilifanyika vizuri kama ilivyopaswa.

baada ya kumalizika kwa zoezi la la kujiandikisha Chama cha Chadema ilimpitisha ndugu Maliwa kuweza kuwania nafasi hiyo ya uwenyekiti wa kijiji. Pia chama cha mapinduzi kiliweza kumpitisha ndugu Kisauni kuweza kugombea nafasi ya uwenyekiti huo.
muda wa kuweka mapingamizi kwa ajili ya wagombea ikapita bila ya kuwepo kwa pingamizi hata moja.

Hatimaye siku ya uchaguzi ikafika, masanduku ya kupigia kura hayakuletwa hali iliyopelekea uchaguzi kutofanyika.chanzo chetu cha habari kinadai kuwa kuna baadhi ya makada wa chama kimoja kikubwa ndio waliopelekea fitna ya kuzuia masanduku ya kura yasiletwe kwa ajili ya uchaguzi huo. hali iliyopelekea watu kuandamana na kufanya vurugu kubwa siku ya jumatatu,gari la diwani wa kata hiyo kupitia CCM, bi Rahel Nyangasa, na gari la kada wa CCM bwana Abdala Dube kuweza kupigwa mawe na kuharibiwa vioo vyote, pia gari la Bi Nyangasa kuweza kutumbukizwa katika mtaro wa maji.

pia katika vurugu hizo baa ya bi Nyangasa iliweza kupigwa mawe na waandamaji na waandamanaji hao waliweza kuchukua vinywaji kutoka katika baa hii, hali iliyopelekea watu kujinywea mipombe kuliko maelezo.

askari wa kikosi cha kutuliza ghasia kutoka mikumi,morogoro na kilosa waliweza kufika eeneo la tukio ili kutuliza ghasia hizo. hadi blog hii inaingia mitamboni askari waliendelea kuwepo ruaha kuendelea kulinda usalama wa eneo hilo

No comments:

Post a Comment