
Hadi kufikia sasa Warembo wapatao 12 kutoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ), na Time, Ustawi wa Jamii na kile cha Usimamizi wa Fedha (IFM), wameisharipoti kambini.
Naye Mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alisema kwamba Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang'anyiro hicho, kwa sasa wanaendelea na zoezi la kujifua ndani ya Hoteli ya Lamada iliyopo hapa Jijini chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku kwa upande wa shoo wakinolewa na Bob Rich.
Si lingine bali ni lile Shindano la kumsaka mlimbwende wa Redd’s Miss Dar Intercollege 2012 linatarajiwa kuwika ndani ya Jkumbi wa Sunciro, ulipo Sinza Shekilango hapa Jijini hapo Juni 8 mwaka huu.
Warembo waliopo kwneye mazoezi hayo ni pamoja na Hilda Edward, Nancy Maganga, Saada Seleman, Neema Nashon, Rose Muchunguzi, Fina Revocatus, Jane Augustino, Theresia Isaya na Natasha Deo. Taji la kitongoji hicho linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM.
Mbali na hilo Mratibu huyo ameziomba Kampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini shindano hilo, ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake na hasa ikizingatiwa kuwa washiriki wake wana vigezo vya hali ya juu.
No comments:
Post a Comment