tuwasiliane

Monday, May 21, 2012

21 MAY.MTOTO WA SHEHE YAHYA ATABILI MABALAA


Mwaka mmoja baada ya kifo cha mtabiri maarufu wa nyota Afrika Mashariki, Sheikh Yahya Hussein, mtoto wake Maalim Hassan ametangaza rasmi kurithi kazi ya baba yake, huku akianza utabiri kwa kusema ndani ya mwaka huu kutatokea vifo vya mawaziri, majaji, mahakimu na wanasheria maarufu.

Aidha, ametabiri mwaka huu kutokea njaa kali kutokana na jua kali na ukame kuikumba nchi, kutokea vifo vya ghafla vya viongozi wa kisiasa waliopo madarakani na viongozi wa dini kukumbwa na kashfa mbaya na za kutisha zitakazovunja hadhi zao.

Kadhalika ametabiri Rais Jakaya Kikwete kupata umaarufu mkubwa wa kisiasa na kushirikisha wapinzani katika shughuli kadhaa za kiserikali, huku amani, utulivu na mshikamano ukiendelea kushamiri Zanzibar.

No comments:

Post a Comment