
Bingwa wa Tanzania Bara Simba SC amerudi msituni kuwinda nyama za mwarabu wa Sudan El Ahly Shandy baada ya kutafuna vilivyo nyama za mtani wake Yanga.
Simba SC inatarajiwa kwenda Sudan siku ya jumatano ya mei 9, ambapo watatoka Dar es salaam saa 8 mchana na kutua Khartoum, Sudan saa 2 usiku wakipitia Kenya.
Mwenyekiti wa Simba SC Muheshimiwa Alhaj Ismail Aden Rage amesema kuwa baada ya kutwa ubingwa jana, walikuwa katika harakati za kukamilisha taratibu zakufika Sudan, ambapo wataondoka jumatano saa 8 mchana kwa shirika la ndege la Kenya Airways.
Rage alisema pia timu yake ya Simba imeanza mazoezi leo ya kusaka makali ya kwenda kuimaliza El ahly Shandy katika ardhi yao.
Simba SC watacheza na El Ahly Shandi mwishoni mwajuma hili.
No comments:
Post a Comment