tuwasiliane

Wednesday, May 2, 2012

02 MAY;BOCCO AWEKA RIKODI AZAM


Juzi jioni mshambuliaji wa Azam FC, John Raphael Bocco 'Adbayor' alifunga goli lake la 22 katika msimu wa 2011/12 na kuweka rikodi ya kufunga magoli mengi katika msimu mmoja ndani ya klabu ya Azam FC.

Nnje ya rikodi hiyo vilevile Bocco aliweka rikodi ndani ya Azam FC ya kufunga magoli mengi katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania Bara 'VPL' ndani ya msimu mmoja kwa kufunga goli la 17 hapo jana katika ushindi wa goli 3-1, walioupata Azam toka kwa Toto Africa ya Mwanza.

Rikodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na mshambualiaji wazamani wa Yanga Mrisho Khalfan Ngassa, ambaye aliifungia Azam FC magoli 16 katika ligi kuu ya msimu wa 2010/11 na Ngassa aliibuka mfungaji Bora.

Bocco amefunga jumla ya goli 17 mpaka sasa katika ligi kuu ya Vodacom na magoli 5 katika michuano ya kombe la Mapinduzi, ambapo timu yake ya Azam FC ilinyakuwa ubingwa wa kombe hilo na Bocco kutwaa ufungaji Bora.

John Bocco amekuwa nguzo muhimu ndani ya kikosi cha Azam FC na ni miongoni mwa wachezaji wachache waliokuwemo katika kupandisha timu daraja na bado wamo kikosini.

John Bocco ndiye mchezaji anaeshikilia usukani katika kuziona nyavu za wapinzani katika historia ya klabu ya Azam FC.

Pamoja na kuziona nyavu kila anapokuwa na uzi wa timu hiyo yenye maskani yake Chamanzi Dar es salaam, amekuwa na wakati mgumu pale anapokuwa na uzi wa Taifa na mapema mwezi jana alitangaza kuacha kuichezea timu ya Taifa akiwa na umri wa miaka 22.

Bocco ana nafasi kubwa ya kuinuka mfungaji bora katika ligi kuu ya Vodacom msimu huu.

No comments:

Post a Comment