tuwasiliane

Wednesday, May 2, 2012

02 MAY. BREAKING NEWZ; MECHI YA AZAM NA MTIBWA KURUDIWA


Mchezo baina ya Azam FC na Mtibwa Sugar FC umeamuriwa kurudiwa na kamati ya Nidhamu iliyochini ya Alfreid Tibaigana kufuatia rufaa ya African Lyon iliyojadiliwa leo katika ofisi za TFF jijini Dar es salaam.

Taarifa zilizotoka katika mkutano huo zinadai kuwa Tibaigana amefuta matokeo ya mchezo huo ulisimama wakati matokeo yakiwa sare ya 1-1 na kamati ya ligi kuipa point 3 na goli 3 Azam FC kutokana na Mtibwa Sugar kudaiwa kuwa chanzo cha mchezo huo kusimamishwa.

Kwa maamuzi hayo sasa Azam FC na Mtibwa Sugar wanahesabika kuwa na mchezo mmoja mkononi ambapo kuna kila dalili ya kuchezwa kiporo hiko nnje ya kalenda ya mwaka wa ligi kuu ya vodacom ambayo inatarajiwa kufungwa mei 5 mwaka huu.

Azam sasa watahesabika kuwa na point 53 nyuma kwa point 6 toka kwa vinara Simba SC wenye mchezo mmoja ziada ya Azam FC na endapo Simba SC wakipoteza mbele ya mtani wake wa jadi kunaipa nafasi Azam FC kuzichanga karata zake vyema katika kiporo hicho endapo wataichapa Kagera Sugar hapo mei 5.

No comments:

Post a Comment