tuwasiliane

Monday, April 30, 2012

30 APR.Hogdson atajwa


Roy Hodgson anatazamiwa kushauriana na chama cha soka cha FA siku ya Jumatatu, ikiwa atakubali kazi ya kuiongoza timu ya taifa ya England.
Roy Hodgson

Hodgson ana ujuzi wa miaka mingi katika kuvifundisha vilabu mbalimbali barani Ulaya

Tangazo la ikiwa ataikubali kazi hiyo litatolewa katika muda usiozidi saa 48.

Chama cha FA kinaeleza kwamba meneja huyo wa klabu ya West Brom, na ambaye ana umri wa miaka 64, ndiye mtu wa pekee ambaye chama kimeshauriana naye moja kwa moja katika kumtafuta atakayemrithi meneja wa awali Fabio Capello.

"Roy ndiye meneja wa pekee tuliyeshauriana naye na kufikia sasa tumezingatia ratiba yetu vyema kama ilivyopangwa tangu mwanzo", alielezea Bernstein.

Hodgson tayari amezungumza na mwenyekiti wa FA, David Bernstein, na sasa anatazamiwa kukutana na bodi kamili ya watu wanne.

Hodgson, ambaye alizaliwa katika mtaa wa Croydon mjini London mwaka 1947, aliwahi kuichezea klabu ya Crystal Palace, Gravesend na Northfleet, Maidstone na vile vile timu ya Afrika Kusini, Berea Park.

Alianza kazi ya ukocha mwaka 1976, alipoifundisha timu ya Sweden, Halmstad.

Amewahi kuzifunza timu za Sweden, England, Uswisi, Italia, Denmark na Norway.

Vipindi viwil alitoa mafunzo pia kwa timu ya Inter Milan ya Italia katika miaka ya tisini.

Aliifundisha timu ya Switzerland katika mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 1994.

Vile vile aliisimamia timu ya Falme za Uarabu, UAE, kuanzia mwaka 2002 hadi 2004, na Finland kati ya mwaka 2005 hadi 2007.

Nchini Uingereza alivifunza vilabu vya ligi kuu ya Premier Blackburn, Fulham na Liverpool, na hatimaye kuhamia West Brom mwezi Februari mwaka 2011.

Awali, hata kabla ya kushauriwa na FA juu ya kazi hiyo, akizungumza na BBC, alisema "atafurahi sana" kuisimamia timu ya England

Siku ya Jumamosi, Bernstein alishauriana na klabu ya West Brom, ambayo ilimpa idhini kuzungumza na Hodgson.

Inatazamiwa iwapo ataupata mkataba huo, ataweza kuiongoza England katika mashindano makubwa matatu yajayo, ikiwa ni pamoja na Euro 2016, miezi miwili tu kabla ya yeye kuadhimisha miaka 69 ya kuzaliwa kwake.

Mkataba wake na West Brom unaendelea hadi tarehe 30 Juni.

No comments:

Post a Comment