tuwasiliane

Thursday, April 26, 2012

26 APR. YANGA YAONA MWEZI

Ligi kuu ya Vodacom iliendelea leo na kushuhudia Mshambuliaji wa Yanga toka Uganda Hamisi Kiiza akiingia kwenye nyavu mara mbili katika ushindi wa goli 4-1 walioupata mbele ya JKT Oljoro. Yanga walikaribishwa na JKT Oljoro katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo Arusha, na Yanga kwenda mapumziko wakiwa teyari wame wakirimu wenyeji wao goli 3-0. Magoli hayo ya kipindi cha kwanza yalifungwa na Mshambuliaji wa Uganda Hamisi Kiiza aliyefunga mawili na kiungo toka Rwanda Haruna Niyonzima. Katika dakika ya 68 ya mchezo JKT Oljoro walipata penati, iliyowapatia goli la kufutia machozi. Kabla ya Mtanzania Pius Kisambale kuhitimisha kalamu ya magoli kwa kuifungia Yanga goli la nne katika dakika ya 81 ya mchezo. Kwa matokeo hayo Yanga wamefikisha point 49 na wamebakisha mchezo mmoja dhidi ya Simba SC utakao pigwa mei 5 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Katika mchezo mwingine uliochezwa katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi Dar es salaam, ulio wakutanisha ndugu wawili JKT Ruvu na Ruvu Shuuting ulimalizika kwa sare ya goli 2-2. Ruvu Shooting walikuwa wa mwanzo kuandika goli katika dakika ya 21, goli ambalo
Masau Sigara aliisawazishia JKT Ruvu katika dakika ya 24. JKT Ruvu waliandika goli la pili kupitia kwa John Mketo kabla ya Jamal Issa kuisawazishia Ruvu Shooting na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya 2-2.

No comments:

Post a Comment