
Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anasakata soka nchini Marekani, Nizar Khalfan anatarajiwa kutangazwa leo kuwa mchezaji wa Simba SC, kwa ajili ya msimu ujao na mashindano ya kimataifa.
Nizar Khalfan kabla ya kujiunga na Vancouver Whitecaps ya Canada alikuwa anachezea Moro United ya jijini Dar es salaam akiwa ametokea Qatar.
Kabla ya kwenda Qatar amepata kuitumikia Mtibwa Sugar na akiwa Marekani alikuwa amesajiliwa na timu ya Philadephia Union akitokea Vancouver ambapo alitemwa Philadephia kabla ya msimu mpya wa ligi kuu ya Marekani kuanza mapema mwaka huu.
Mwenyeketi wa Simba SC Muheshimiwa Alhaj Ismail Aden Rage amesema kuwa mchezaji huyo atatambulishwa leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaama katika kipindi cha mapumziko wa mchezo kati ya Simba na Moro united utakao chezwa kesho kuanzia saa 10 na 30.
No comments:
Post a Comment