
Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Yanga wamezinduka leo baada ya kuwachapa Polisi Dodoma goli 3-1 katika muendelezo wa ligi kuu ya Vodacom hii leo katika uwanja wa Taifa.
Yanga walianza kuhesabu goli la kwanza kupitia kwa Davis Mwape kabla ya Idrisa Rashid Senga kuipatia yanga goli la pili, na Mwape kukamilisha kwa kuifungia goli la 3 yanga.
Katika mchezo wa leo mashabiki wa Yanga walijitokeza wa chache ukilinganisha na michezo mingine ya yanga.
No comments:
Post a Comment