Tuesday, April 17, 2012
17 APR. Milovan awa 'mbogo'
KOCHA wa Simba, Milovan Cirkovic mwishoni mwa wiki aligeuka 'mbogo' kwa winga wake Salum Machaku aliyeshindwa kufutwa maelezo yake kila dakika.
Katika mtanange huo uliopigwa kwenye dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.
Mara kwa mara Milovan alionekana akinyanyuka kwenye benchi lake na kwenda kumfokea Machaku kitendo ambacho baadhi ya mashabiki uwanjani walikitafsiri pengine ni kutoridhishwa na uchezaji wake.
Jambo la kushangaza zaidi lilionekana baada ya mwamuzi wa pambano hilo Rashid Msangi kupuliza kipenga cha mapumziko, Milovan alinyanyuka kwenye bechi na kumfuata moja kwa moja Machaku ndani ya uwanja na kuanza kumfokea.
Hata hivyo, juhudi za Cirkovic kumekebisha Machaku ziligonga mwamba baada ya kuamua kumtoa dakika ya 68 na nafasi yake kuchukuliwa na chipukizi Edward Christopher.
Akiezelezea kwa undani sababu za kuonekana akimfokea mara kwa mara Machaku, bosi huyo raia wa Serbia alisema:
"Mimi nilimpanga Machaku na Okwi(Emmanuel) wacheze pembeni na niliwapa maelekeo yote, majukumu yake yalikuwa ni kupiga krosi.
"Tatizo ni kwamba alikuwa akipuuza nilichomwambia kwani alikuwa anaingia ndani kucheza kama kiungo wakati si kazi yake, huu ni ujinga ni lazima awe msikivu,"aling'aka Circovic.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment