tuwasiliane

Saturday, April 14, 2012

14 APR.Rufaa ya Yanga wiki ijayo


WAKATI mechi za Ligi Kuu zikiendelea leo na kesho kwenye viwanja tofauti, rufaa ya Yanga iliyokuwa isikilizwe leo na Kamati ya Nidhamu ya Shrikisho la Soka Tanzania (TFF), imesogezwa mbele mpaka ijayo April 17.

Yanga ilikata rufaa kupokwa pointi tatu na Kamati ya Ligi kufuatia kumchezesha Nadir Haroub aliyekabiliwa na adhabu ya kutocheza mechi tatu baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwenye mechi dhidi ya Azam FC wiki mbili zilizopita.

Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bonifance Wambura alisema jana jijini Dar es Salaam kwamba, kikao hicho sasa kitafanyika wiki ijayo lakini bila kutoa sababu.

Hata hivyo, Ofisa habari wa Yanga, Louis Sendeu alisema jana kuwa wanashangazwa na uamuzi ya kamati hiyo ya nidhamu juu ya adhabu ya Haroub.

"Sisi tuliomba ufafanuzi kuhusu adhabu hii yenye utata. Wametumia kifungu cha 25 (C) kwa kosa la kumpiga mwamuzi, sisi tumekata rufaa kwa vile mchezaji huyo hakumpiga mwamuzi," alisema Sendeu.

"Waliofanya vile wanafahamika, Horoub hakuonyesha kadi nyekundu kwa kosa la kufanya fujo na siyo kumpiga mwamuzi kama inavyoelezwa," alisema zaidi.

"Na sisi tumetumia kanuni hiyo hiyo ya 25 kutaka ufafanuzi, hatuwezi kukubali pointi zipotee, kufanya fujo na kupiga ni vitu viwili tofauti," aliongeza.

Hata hivyo kanuni hiyo ya 25 (b), inayozungumzia udhibiti wa wachezaji inasema mchezaji atakayetolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja atakosa michezo miwili.

No comments:

Post a Comment