tuwasiliane

Wednesday, April 11, 2012

11APR. Yanga kamili yaenda kanda ya Ziwa


Kikosi cha Mabingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ambao pia ni mabingwa wa ligi kuu nchini timu ya Young Africans kimeondoka alfajiri ya leo kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya kucheza mchezo wake wa ligi kuu ya Vodacom nchini Tanzania bara nchini dhidi ya timu ya Toto Africans, mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.

Young Africans ambayo inahitaji ushindi katika mchezo huo wa jumapili ili kuweza kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wake, imeondoka kwa njia ya usafiri wa ardhini ambapo timu leo moja kwa moja itafika mjiini Kahama ambapo kesho siku ya alhamis itacheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kahama Amabassador katika uwanja wa Taifa mjini hapo, uwanja uliopo maeneo ya Majengo mapya.

Mabingwa hawa wameamua kupitia mjini Kahama kucheza mchezo wa kirafiki, kufuatia wapenzi na washabiki wa timu hiyo wa wilayani humo kuomba timu ipite huko ili waweze pata nafasi ya kuwaona wachezaji wao amabao wamekuwa wakiwasikia tu na kuwatazama kwa luninga.

Uongozi uliona ni busara timu ikapita huko kama yalivyokuwa maombi ya wapenzi wa soka wa wilaya hiyo yenye watu wengi na biashara nyingi katika ukanda wa ziwa victoria, wapenzi wa soka kutoka miji ya Geita, Ushirombo, Nzega, Ngara, Biharamulo na miji ya karibu wanatazamiwa kuhudhuria mchezo huo hapo kesho.

Mara baada ya mchezo huo wa kesho, Young Africans itaondoka ijumaa asubuhi kuelekea jijini Mwanza, ambapo itafanya mazoezi siku ya ijumaa jioni na jumamosi jioni kabla ya pamabano litakalofanyika siku ya jumapili.

Mara baada ya mchezo wa jumapili dhidi ya Toto Africans Young Africans itaelekea mjini Bukoba ambapo itacheza na timu ya Kagera Sugar siku ya jumatano kabla ya alhamis kurudi jijin Mwanza na kuanza safari ya kurudi jijini Dar es salaam.

Yanga imeondoka na kikosi cha wachezaji wa 23 ambao ni:
Walinda Mlango: Yaw Berko, Shaban Hassan Kado, Said Mohamed.

Walinzi wa Pemebeni: Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Oscar Joshua, Abuu Ubwa, Walinzi wa Kati: Chacha Marwa, Zubery Ubwa, Bakari Mbega, Athumani Iddy Chuji

Viungo Wakabaji: Juma Seif Kijiko, Ibrahim Job, Godfrey Bonny,
Viungo Washambuliaji: Haruna Niyonzima, Rashid Gumbo Washambuliaji wa pembeni: Shamte Ally, Idrisa Rashid, Kiggi Makasi, Washambuliaji: Davies Mwape, Kenneth Asamoah, Hamis Kiiza, Pius Kisambale

No comments:

Post a Comment