Monday, April 9, 2012
09 APR.SIMBA WATUA SALAMA DAR, WAANZA KUIVUTIA KASI EL AHLY SHANDY
KIKOSI cha Simba SC kimewasili salama Dar es Salaam alfajiri ya leo, wakitokea Algeria ambako waliitioa ES Setif ya huko katika Kombe la Shirikisho kwa faida ya bao le ugenini baada ya sare ya 3-3.
Wapenzi na wanachama wa Simba walimiminika kuilaki timu yao, lakini mapokezi hayakuwa makubwa kama ilivyotarajiwa kutokana na muda na pili msiba wa mwigizaji Steven Kanumba.
Simba sasa imefuzu hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho la Soka CAF, kwa licha ya kufungwa mabao 3-1 na ES Setif kwenye Uwanja wa Mei 8, mjini Setif katika mchezo wa marudiano jana usiku.
Shukrani kwake mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Arnold Okwi aliyefunga bao la dakika za lala salama wakati refa amekwishaonyesha dakika za majeruhi tano.
Katika mchezo huo, Simba ilipata pigo mapema dakika ya 18 baada ya beki wake Juma Said Nyosso kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kucheza ‘rafu ya wazi’.
Hadi mapumziko, tayari Setif walikuwa mbele kwa mabao 2-0 na mapema kipindi cha pili, wakapiga la tatu.
Mchezo wa kwanza Simba ilishinda 2-0 Dar es Salaam na sasa itamenyana na Al Ahly ya Sudan.
Simba sasa baada ya kuitoa ES Setif imeingia hatua ya mwisho ya mchujo ambako itamenyana na ama El Ahly Shandy ya Sudan na itaanzia nyumbani, mechi ya kwanza ikichezwa Aprili 29, kabla ya timu hizo kurudiana wiki mbili baadaye Sudan.
Simba ikifanikiwa kuitoa El Ahly Shandy, moja kwa moja itafuzu kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ikiwa timu ya kwanza ya Tanzania kucheza hatua hiyo.
Tanzania imewahi kufikisha katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa tu, mara mbili mwaka 1998 Yanga na 2003 Simba wenyewe.
Mwaka 2007 Yanga ilikaribia kuingia hatua ya makundi ya Makundi ya Kombe la Shirikisho, lakini ikatolewa na El Merreikh ya Sudan, wakati mwaka jana pia Simba ilikaribia kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo, ikatolewa na Daring Club Motema Pembe ya DRC.
Kama wakifanikiwa kufika hatua ya makundi ya michuano hiyo, Simba watapewa donge nono la dola za Kimarekani 150, 000, zaidi ya Sh. Sh Milioni 250,000 za Tanzania.
FEDHA ZINAZOWASUBIRI SIMBA SC:
NAFASI: KLABU TFF
Ubingwa $625 000 $35 000
Fainali $ 432 000 $ 30 000
Nafasi ya 2 kundini $ 239 000 $ 25 000
Nafasi ya 3 kundini $ 239 000 $ 20 000
Nafasi ya 4 kundini $ 150 000 $ 15 000
Source: bongostaz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment