tuwasiliane

Sunday, April 8, 2012

08 APR. HATIMAYE LULU AZUNGUMZA ASEMA HAKUMSUKUMA KANUMBA


Baada ya kugoma kutoa maelezo kwa takribani siku nzima ya jana, mwanadada Lulu hatimaye amezungumza na polisi na kuelezea kilichotokea baina yake na marehemu Steven Kanumba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema Kanumba alikufa kutokana na ugomvi uliotokea kati yake na rafiki yake wa kike Lulu.

"Kanumba amefariki usiku wa kuamkia leo (jana) majira ya saa tisa usiku, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ugomvi kati yake na rafiki yake wa kike anayejulikana kwa jina la Elizabeth Michael 'Lulu' mwenye umri wa miaka 18.

Alisema kabla ya ugomvi huo kutokea kati yao wakiwa chumbani, simu ya Lulu iliita na akaamua kutoka nje kupokea kitendo kilichomuudhi Kanumba.

Kamanda Kenyela alisema Kanumba aliamua kumfuata Lulu nje huku akifoka kwa sauti akitaka aelezwe kwanini alitoka nje kupokea simu huku akimtuhumu kuwa huenda alikuwa akizungumza na mwanaume mwingine.

Aliongeza baada ya Lulu kuona Kanumba akimfuata aliamua kukimbia kutoka nje ya geti , lakini kabla hajafanikiwa kufungua geti, Kanumba alimkamata na kumrudishwa ndani.

Kamanda Kenyela, alisema Kanumba akiwa amemshikilia waliingia wote chumbani na kufunga mlango.

Hata hivyo, alisema haijulikani nani aliyefunga mlango, ingawa maelezo ya Lulu anadi kuwa aliyefunga mlango ni Kanumba.

Kamanda huyo alisema Lulu anaeleza kuwa baada ya Kanumba kufunga mlango, alimuona akilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta wa chumba hicho kabla ya kuanguka chini.

Alibainisha kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Kanumba alikuwa amekunywa Whisky (pombe kali) aina ya Jacky Daniel, hata hivyo, bado wanachunguza zaidi kujua kama kweli Kanumba alilegea tu na kuanguka, ama alipigwa na kitu kizito kichwani au alisukumwa kwa nguvu na kumfanya aangukie kisogo.

“Uchunguzi ukikamilika tutampeleka mahakamani kwa tuhuma za mauaji,” aliongeza Kamanda Kenyela.

UPDATES;Masaa machache baada ya mama mzazi wa Kanumba kufika Dar es Salaam akitokea kwao Bukoba amesema kwamba amekubaliana na maombi ya wapenzi wa mwanae na wanabongo movie kwamba mwanae azikwe hapa hapa Dar.

Hivyo Kanumba atazikwa makaburi ya kinondoni na ataagwa siku ya jumanne katika viwanja vya leaders kinondoni.

SOURCE SHAFFIH DAUDA

2 comments:

  1. Kifo Cha Kanumba kwa kweli kiustua Umma wa wa-Tanzania na sasa hata mambo kama kuundwa kwa tume ya kukusanya marekebisho/mabadliko ya Katiba yamewekwa kando kabisa.

    ReplyDelete
  2. DA KWELI BABA MZAZI CHANDE,HATA USHINDI WA SIMBA UMESAHAULIKA

    ReplyDelete