tuwasiliane

Thursday, April 5, 2012

05 APR. BREAKING NEWZ; MAHAKAMA KUU YATENGUA MATOKEO YA UBUNGE JIMBO LA ARUSHA


HABARI AMBAZO TUMEZIPATA HIVI PUNDE MAHAKAMA KUU,IMETENGUA MATOKEO YA UBUNGE KATIKA JIMBO LA ARUSHA MJINI

JIMBO HILO AMBALO KATIKA UCHAGUZI ULIOFANYIKA MWAKA 2010 MGOMBEA WA CHADEMA BWANA GODBLESS LEMA ALIIIBUKA KIDEDEA KUMWAGA MGOMBEA WA CCM DR BARTILDA BULHANI
Uamuzi huo umefikiwa leo Aprili 5, 2012 mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha hilo yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo.


Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).


Wanachama hao wanadai kuwa taratibu za maadili ya uchaguzi zilikiukwa wa kuwa mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli katika mikutano ya kampeni aliyofanya jimboni Arusha.


Katika kesi hiyo wadai walileta mashahidi 14 kwenda kutoa ushahidi wao katika mahakama hiyo nawadaiwa walifanikiwa kuwaleta mashahidi 5
kujitetea.


Kuvuliwa Ubunge kwa Lema, kuna kuja siku chache wakati bado cham hicho kipo katika shamra shamra za ushindi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki mkoani humo.


KWA HALI HIYO JIMBO LA ARUSHA MJINI SASA LIPO WAZI

KWA HABARI ZAIDI ENDELEA KUSOMA BLOG YAKO PENDWA RUTAENDELEA KUKUJUZA ZAIDI NA RIPOTI YA HUKUMU YA MAHAKAMA KUU

No comments:

Post a Comment