Kikosi cha Simba SC kimetuwa salama Cairo nchini Misri wakiwa safarini kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa marejeano wa kombe la shirikisho CAF dhidi ya ES-Setif ya Algeria siku ya ijumaa ya April 6 mwaka huu.
Katika msafara huo wa simba uliwajumuisha Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba Damian Manembe na Ofisa Habari, Ezekiel Kamwaga.
Wengine ni Kocha Mkuu, Milovan Cirkovic, Kocha Msaidizi Amatre Richard, kocha wa makipa James Kisaka, daktari wa timu Cosmas Kapinga, Meneja Nico Nyagawa na mtunza vifaa Kessy Rajab.
Wachezaji waliopo kwenye msafara ni Juma Kaseja, Ally Mustafa, Nassor Masoud, Shomari Kapombe, Amir Maftaha, Juma Nyoso, Kelvin Yondani, Victor Costa, Obadia Mungusa, Jonas Mkude, Patrick Mafisango, Mwinyi Kazimoto, Haruna Moshi, Salum Machaku, Uhuru Suleiman, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi, Edward Christopher, Derick Walulya na Gervais Kago.
Katika mchezo wa kwanza Simba SC walishinda goli 2-0 katika uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment