
Aliweza kutamba kwa kumshushia kichapo Mbwa mwizi yaani mpinzani wake Francis Cheka ‘SMG’ wa Morogoro kwenye pambano lao litakalofanyika kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam, Aprili 28, mwaka huu.
Si mwingine bali ni Bondia wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Mada Maugo, ‘Mbunge wa Musoma’ na katika pambano hilo mabondia hao walioko kwenye kiwango cha juu hivi sasa hapa nchini, wanawania mkanda wa ubingwa wa IBF, pamoja na gari aina ya Toyota lenye thamani ya sh milioni 8.
Maugo alisema anashukuru sana kitendo cha kubadilishiwa waamuzi, kwani alijua wakiwepo waamuzi waliozoeleka siku zote hapa nchini, hataweza kupata ushindi kutokana na kutowaamini.
“Kitendo cha kupewa waamuzi kutoka nje ya nchi ni ushindi kwangu, maana waamuzi wa Bongo huwa hawanitendei haki siku zote, hivyo nawaomba mashabiki wangu mjiandae kunipongeza kwa ushindi,” alisema Maugo.
Pia aliwataka wadau mbalimbali wa mchezo huo nchini, kujitokeza kwa wingi katika ukumbi huo ili kumpa nguvu na kushuhudia mikono inavyofanya kazi yake
No comments:
Post a Comment