
Magoli mawili kwa upande wa simba ambayo yalifungwa na Salum Machaku na Haruna moshi boban kwenye mchezo dhidi ya African Lyon,yameweza kuizidisha kung`aa kileni mwa liki kuu ya Vodacom
katika mchezo huo magoli yote ya simba yalipatikana katika kipindi cha kwanza.katika kipindi hicho simba walionekana kutawala vilivyo huku vijana wa Afrikan lyon walikuwa wakicheza mchezo wa kujihami zaidi
katika kipindi cha pili kila timu ilionekana kutaka kubadilisha hali ya mchezo kwa simba kuongeza magoli na Lyon kusawazisha lakini mchezo ulionekana kubalance na hadi mwisho matokeo yakabaki 2kwa simba na 0 kwa Afrikan lyon
KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI TANGA
goli lililofungwa na Hamisi kiiza kwa kichwa katika dakika ya 42 ya mchezo iliiwezesha yanga kuibuka na ushindi wa Goli 1-0 dhidi timu ya Coast union
kwa matokeo ya mechi za leo simbaimeendelea kuaa kileleni mwa ligi hiyo kwa kuwa na points 50 ikifuatiwa na timu ya Yanga ambayo imefikisha points 46 huku azamu ikishuka kwa nafasi moja hadi nafasi ya 3 kwa kuwa ina points 44
ligi hiyo ya vodacom itaendelea tena kesho kwa mchezo kati ya AZAM dhidi ya timu ya jkt ruvu mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa azam chamazi
No comments:
Post a Comment