tuwasiliane

Monday, March 26, 2012

26 MARCH.TFF: Mwasika hana hatia



Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF, imeridhia kitendo alicho kifanya Mchezaji wa timu ya Taifa na Dar Young Africans 'Yanga' Stephane Mwasika kwa kumtoa kwenye kifungo cha mwaka mmoja mpaka kuwa huru kuitumikia klabu yake katika mchezo wa machi 31 dhidi ya Coastal Union.

Mwasika alimpiga mwamuzi Israel Nkongo katika mchezo kati ya Yanga na Azam FC, uliokuwa na fujo ndani yake. Mwasika, Jerry Tegete, Omega Seme, Nadir Haroub na Nurdin Bakari walitiwa kifungoni na kamati ya Ligi, ambapo vifungo hivyo vimetenguliwa na kamati ya nidhamu iliyo kutana jana machi 24.

Kamati ya ligi ilitoa adhabu ya kumfungia mchezaji Stephano Mwasika mwaka mmoja kutocheza mpira na faini ya Tsh milioni moja. Jeryson Tegete alifungiwa kutocheza ligi kuu kwa miezi sita (6) na faini ya sh.500,000.

Wakati Nadir Haroub Cannavaro alifungiwa kutocheza ligi kuu kwa mechi sita (6) na faini ya sh.500,000. Nurdin Bakari na Omega Seme walifungiwa kutocheza mechi tatu (3) za ligi kuu na faini ya sh.500,000.

No comments:

Post a Comment