
Michezo ya ligi kuu ya vodacom imeendelea kwa michezo miwili, ambapo Yanga na Simba wameibuka na ushindi wa goli 1-0.
TAIFA
Goli lililofungwa na kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar Kiggi Makasi katika dakika ya 43 kipindi cha kwanza ilitosha kuwanyamazisha African Lyon katika uwanja wa Taifa.
Yanga ambayo leo walichezesha kikosi cha pili huku beki Shadrack Nsajigwa akicheza nafasi ya kiungu ilipoteza nafasi kadhaa za kujipatia magoli kupitia kwa Davis Mwape na Shamte Ally.
JAMHURI DODOMA
Kiungo toka Rwanda mwenye asili ya Congo Patrick Mutesa Mafisango aliibuka shujaa wa Simba SC baada ya kuipatia goli pekee la ushindi katika dakika ya 46.
Mafisango alifunga goli hilo akiunga krosi ya Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emanuel Okwi mwenye magoli 9.
MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Simba SC (20) 44
2. Azam FC (20) 41
3. Yanga SC (19) 40
4. Mtibwa Sugar (20) 34
5. JKT Oljoro (21) 28
6. JKT Ruvu (20) 27
7. Coastal Union (20) 26
8. Kagera Sugar (21) 24
9. Ruvu Shooting (20) 24
10. African Lyon (18) 18
11. Moro United (21) 18
12. Toto Africa (20) 17
13. Polisi Dodoma (21) 17
14. Villa Squad (19) 16
No comments:
Post a Comment