
Ac Milan Kutovaa Jezi Nyeusi Tena
CEO wa Ac Milan Adriano Galliani amesema kwamba kamwe hawatavaa tena jezi Nyeusi walizovaa kwenye mechi dhidi ya Arsenal katikati ya wiki hii na Kudai kuwa ni bora warudie kuvaa jezi zao za njano na ziwe kama ndio jezi zao kwenye mechi za ugenini.
Mkurugenzi huyo wa Ac Milan(Galliani) amethibitisha mabingwa hao wa ligi ya Sirie A hawatavaa tena jezi hizo nyeusi kwa kuziona kama zina gundu wakati timu hiyo ilipofungwa na Arsenal goli 3-0 kwenye ya Klab bingwa barani Ulaya.
Galliani anaamini jezi hizo nyeusi ndio zilizoleta mkosi na kupelekea Ac milan kupata kipigo hicho,hivyo kuamua kutaka kurudia jezi zao za njano kwenye mechi za Ugenini msimu ujao.
“Hatutavaa jezi zile tena.Nilijaribu kadri ya uwezo wangu na madaraka niliyokua nayo ili kuweza kuepuka lakini ilitubidi tuzivae dhidi ya Arsenal,Lakini njia mbadala ilikua labda tucheze bila jezi”Galliani aliliambia gazeti la nchini Italia La Gazzetta dello Sport.
No comments:
Post a Comment