tuwasiliane

Monday, March 5, 2012

05 MARCH. Simba SC yaichapa Kiyovu, kucheza na Es setif machi 25


Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Simba SC itakutana Es Setif ya Algeria katika raundi ya kwanza ya kombe la shirikisho ambapo Simba SC wataanzia nyumbani kati ya machi 23-25.

Simba wamefika katika hatua hiyo kufuatia ushindi wa goli 2-1 walioupata hii leo mbele ya Kiyovu ya Rwanda katika uwanja wa Taifa, hivyo Simba kuwaondoa Kiyovu katika mashindano ya kombe la shirikisho CAF kwa jumla ya goli 3-2 kufuatia sare ya 1-1 katika mchezo wa awali.


Mchezo huo wa leo ulianza taratibu huku kila timu ukiweka mpira chini na kupiga pasi fupi fupi, na sehemu kubwa ya mchezo ukichezwa katika ya uwanja, huku zikitengenezwa nafasi chache katika kipindi cha kwanza, ambapo Kiyovu walitengeneza moja huku Simba wakitengeneza tatu.

Katika dakika ya 17 mchezaji wa Kiyovu aliangushwa katika eneo la hatari na mwamuzi akipeta na ndipo alipo pigiwa pasi ndefu Emanuel Okwi akiwa upande wa kushoto na kukusanya mabeki kabla ya kumpatia Felixs Sunzu ambaye aliiandikia goli la kuongoza Simba katika dakika ya 18.


Goli la Sunzu uliongeza kasi kidogo mchezo huku Simba SC ikiongeza utulivu na kuweka mpira chini, huku upate wa Kushoto kwa Simba ikionekana kichochoro kwa Kiyovu na kuwa eneo la hatari kwa Simba kupeleka mashambulizi ambapo walikuwa wanacheza Amir Maftah na Emanuel Okwi katika kipindi cha kwanza.

Amir Maftah alipiga pasi iliyomkuta Emanuel Okwi na kukusanya mabeki wa Kiyovu na kuingia katika eneo la hatari akiwa katika kona ngumu kufunga na kupiga pasi ya aina ya V na kumkuta Felix Sunzu na bila ajizi akaipatia Simba goli la pili katika dakika ya 32. Na mchezo kwenda mapumziko Simba wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Kipindi cha pili Kiyovu waliingia kwa dhamira ya kutafuta goli, huku Simba wakiendeleza kandanda lao, huku wakizuia zaidi na Okwi kuingia kati na Mafisango kurejea kushoto ambapo kuliwazibia mwanya Kiyovu kutengeneza mashambulizi kupitia upande huo.

Katika dakika ya 78 mabeki wa Simba walitolewa usingizini baada ya Kiyovu kujipatia goli la kufutia machozi. Mpaka mwisho wa mchezo Simba 2-1 Kiyovu, hivyo Simba kuwa timu pekee toka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyo salia katika mashindano ya CAF.

Kikosi cha Simba leo: Juma Kaseja, Nasor Chollo, Amir Maftah, Juma Nyoso, Kelvin Yondani, Shomari Kapombe, Haruna Moshi/Singano 'Messi', Mwinyi Kazimoto/Jonas, Felix Sunzu/Costa, Patrick Mafisango, Emanuel Okwi

No comments:

Post a Comment