tuwasiliane

Thursday, March 1, 2012

01 MARCH.WBC yamuwekea kikwazo Chisora


Mwanamasumbwi wa Uingereza Dereck Chisora amesimamishwa kwa mda mrefu na chama cha masumbwi World Boxing Council kwa tabia mbovu kabla na baada ya pambano lake la uzani wa juu na Vitali Klitschko.

Mwanamasumbwi huyo wa uzani wa juu wa Uingereza alihusika katika purukushani na Muingereza mwenzake David Haye wakati akihutubia wandishi wa habari baada ya kupoteza pambano mjini Munich Ujerumani.

Vilevile Chisora alimzaba kofi mpinzani wake Klitschko wakati wa vipimo na kumtemea mate mdogo wake Wladmir kabla ya pambano.

Shirika la ndondi '' WBC limesema kua ''mojapo ya tabia mbovu kuwahi kuonyeshwa na mwanamasumbwi ya kulipwa".

Shirika hilo limemtaka Chisora, mwenye umri wa miaka 28, ajaribu kupata matibabu ya jinsi ya kuzuia ghadhabu kabla ya kumuondolea kikwazo.

Rais wa shirika hilo, Jose Sulaiman, amesema mamlaka hayo pia yatatizama jinsi ya kumuwekea adhabu ya faini mcheza ngumi huyo mzaliwa wa Zimbabwe.

Chisora vilevile ataondolewa kwenye orodha ya shirika hilo ambapo anashikilia nambari 14.

Taarifa ya shirika hilo imesema kua inashutumu vikali tabia mbovu ambazo hazikubaliki kwa hali yoyote ile katika mchezo wa masumbwi na kua shirika hilo litachukua hatua za vikwazo na kumtoza pesa mhusika endapo litampata na hatia.

Chini ya utaratibu na nyenzo za shirika hilo, mwanamasumbwi na mstaarabu ambaye ni mfano kwa ulimwengu mzima atakayestahmili matokeo ya pambano kabla na baada ya pigano.

Chisora alitishia kumpiga risasi Haye baada ya mfarakano baina yao mbele ya vyombo vya habari na baadaye alishikiliwa na polisi wa Ujerumani, ingawa baadaye aliachiliwa bila kufunguliwa kesi.

No comments:

Post a Comment