
Baraza la utawala wa kijeshi nchini Misri limetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa baada ya watu wasiopungua 74 kuuwawa katika mapigano kati ya mashabiki wa timu pinzani katika mji wa Port Said
Mamia kadhaa walijeruhiwa wakati mashapiki waliuvamia uwanja baada ya mechi kati ya timu mbili zinazoongoza kwenye ligi al-Masry na al-Ahly.
Mikutano ya dharura ya baraza la mawaziri pamoja na bunge imeitishwa.
Maandamano yamepangiwa kufanyika Alhamisi kulaani hatua ya polisi kutochukua hatua yoyote kuzima fujo hizo.
Mechi zote za ligi kuu nchini Misri zimeahirishwa kwa muda usiojulikana.
Mmoja wa mashabiki wa klabu ya al-Ahly ameiambia BBC kwamba mashabiki wenzake wataandamana kutoka makao makuu ya klabu hiyo mjini Cairo hadi katika afisi za wizara ya mambo ya ndani.
WAKATI HUOHUO Nchini Misri Waandamanaji wamerejea katika mitaa ya mji mkuu Cairo kuonyesha hasira yao juu ya maisha yaliyotokomea jana kwenye mashindano ya mchezo wa mpira wa miguu.
Watu sabini na wanne walipoteza maisha yao katika uwanja wa mpira ulio katika mji wa kaskazini mashariki wa Port Said.Mamiya wengine walijeruhiwa.
Kwenye kikao cha dharura cha bunge, Waziri mkuu wa nchi hio ametangaza kua wanakamati wa Chama cha mpira cha nchi hio wote wamefutwa kazi na wanachunguzwa. Gavana wa mji wa Port Said amejiuzulu.
Waziri Mkuu wa Misri Kamal Ganzouri ametangaza hatua ya kuwafuta kazi wanachama wote wa chama cha mpira cha Misri na kujizulu kwa baadhi yao kwenye Kikao cha dharura cha Bunge.
Hatua hio hata hivyo huenda isitoshe kuwaridhisha Wamisri wengi. Kuna dalili la kuongezeka kwa ghadhabu ya wa Misri juu ya Wizara ya mashauri ya nchini inayosimamia Polisi, ambayo wengi wanahisi haijabadilika tangu enzi za Hosni Mubarak.
No comments:
Post a Comment