tuwasiliane

Wednesday, February 29, 2012

29 FEB.Scott Parker ndiye nahodha wa England


Mcheza kiungo wa klabu ya Tottenham Scott Parker ataongoza Timu yake ya taifa kama nahodha kwa pambano la kirafiki dhidi ya Uholanzi kwenye uwanja wa Wembley.

Kocha msimamizi Stuart Pearce amemteua Parker badala ya orodha yenye majina kama Steven Gerrard wa Liverpool na James Milner wa Manchester City na Joe Hart.

Parker, mwenye umri wa miaka 31, ameiwakilisha Timu ya Taifa mara 10 tangu mwaka 2003 na mwaka 2011 alijitokeza mara saba katika mechi 9.

Mapema wiki hii alichaguliwa na mashabiki kama mchezaji bora wa mwaka jana nchini England.

Scott Parker ni mcheza kiungo anayetumia maguvu na ngwara, na ni mwaka jana nyota ya mchezaji huyu iliposhamiri mno.

Kati ya mwaka 2003 na 2010, aliweza kuichezea Timu ya Taifa mara tatu ingawa alihama mara tatu kutoka vilabu - Charlton, Chelsea na Newcastle.

Mwaka jana baada ya kuibuka mchezaji bora wa wandishiw a habari za soka kwa mchango wake kwa klabu ya West Ham iliyoshuka daraja alijiunga na klabu ya Tottenham kwa kitita cha pauni £5.5m.

Katika pambano la hivi karibuni mchezaji huyu alionyeshwa kadi mbili za njano kwa utumiaji wake nguvu wakati wa pambano lenye sifa ya uhasama mkubwa wa vilabu viwili vya eneo la kaskazini mwa London, Arsenal na hivyo hatoshiriki pambano muhimu la klabu yake dhidi ya Manchester United siku ya jumapili ijayo.

No comments:

Post a Comment