tuwasiliane

Wednesday, February 29, 2012

29 FEB. BREAKING NEWZ;Afyeka nyeti zake, kisa MADEMU!


Kijana Priva Elian wa Rombo mkoani Kilimanjaro, amefyeka sehemu zake za siri na kuziondoa, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kugombaniwa na wanawake wawili.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walidai kijana huyo alifikia uamuzi huo baada ya wanawake wawili kumgombea.

Walidai kuwa alifikia uamuzi huo Februari 27, mwaka huu saa 1:30 asubuhi baada ya kupandwa na ghadhabu kutokana na usumbufu mwingi aliokuwa akiupata kutoka kwa wanawake hao.

Walieleza kuwa mara baada ya kuchukua uamuzi huo, alimwita mdogo wake ambaye hakutambulika jina na kumweleza kuwa achukue viungo hivyo na kuwapelekea wanawake hao ili wavigombee.

“Hatujui alitumia kifaa gani kujifyeka kwani kinaonesha ni kikali sana, kwani baada ya kukata sehemu hizo nyeti, alimpa mdogo wake ili awapelekee wanawake hao kwani ndicho kitu muhimu kwao na siyo yeye,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo la kusikitisha.

1 comment:

  1. Naamini amechanganikiwa mimi nampa pole sana kwani halikuwa jawabu la busara kwake kuhatarisha maisha yake kwa kuvuja damu nyingi kwaajili ya wabibi.

    ReplyDelete