tuwasiliane

Tuesday, February 28, 2012

28 FEB. KIYOVU YAIFICHA SIMBA SIKU YA KUWASILI


UONGOZI wa Simba umesema haujui ni lini wapinzani wao Kiyovu watawasili nchini, huku viingilio vya mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho vikiwa ni shilingi 5,000 na 50,000.

Simba watashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi kuwakabili Kiyovu wakiwa kumbukumbu ya kulazimishwa sare 1-1 jijini Kigali nchini Rwanda.

Akizungumza jijini jana Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema maandalizi yote yamekalimika lakini hawajapokea taarifa za ujio wa Kiyovu.

Kamwaga alisema mpaka sasa hawana mawasiliano yoyote lini timu hiyo itawasili nchini.
Habari ambazo gazeti hili limezipata zinasema kuwa Kiyovu watawasili nchini Alhamisi siku moja baada ya kumalizika kwa mechi za kimataifa kwa kuwa nyota wake watatu wataichezea Rwanda kesho dhidi ya Nigeria.

Mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi Yabarow Hagi Wiish na wasaidizi wake Aweis Ahmed Nur na Abdirahman Omar Abdi, wote kutoka Somalia.

Katikati hatua nyingine viingilio kwenye mchezo huo vinategemewa kuanzia sh 50,000 kwa vip na kile kidogo ni sh 5,000.

Kamwaga alisema suala la viingilio vya mchezo huo vitawekwa bayana kesho (leo).
"Tutatoa utaratibu wa kukaa uwanjani kwani tunataka kubadilisha utaratibu ili kila mtu aweze kufurahia alipokaa kulingana na kiingilio alichotoa tofauti na sasa," alisema.

Wakati huohuo; Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limethibisha mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Zamalek na Yanga itachezwa Machi 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jeshi jijini Cairo kuanzia saa 12 jioni kwa saa za Misri.

Kwa mujibu wa maelekezo ya CAF mechi hiyo itachezwa bila washabiki kwa vile Zamalek inakabiliwa na adhabu ya kucheza mechi hiyo bila washabiki.

Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco ambao ni Jihed Redouane, Rouani Bouazza na Bekkali Mimoun wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Gihed Greisha wa Misri. Kamishna wa mchezo huo ni Ben Khadiga wa Tunisia.

No comments:

Post a Comment