Friday, February 24, 2012
24 FEB. Ni kweli Mwasikili kubaniwa na TFF?
Kwani kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Nyota huyo kurudishwa nchini kinyemela, halimiliyozua maswali miongoni mwa wadau wa Soka kutokana na kuenea kwa habari kwamba wamerudishwa kutokana na kuchelewa kupewa hati hiyo kama inavyodaiwa.
Kwani Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliwezakufafanua kwamba nahodha wa timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania 'Twiga Stars' Sophia Mwasikili, aliyepata nafasi ya kucheza soka ya kulipwa nchini Uturuki katika klabu ya Luleburgazgucu Spor Kulubu, amerudishwa mchini kutokana matatizo ya viza na si Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
Naye Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema nyota huyo amerudishwa baada ya kubainika kuwa viza aliyoondokana nayo nchini ilikuwa ni ya kibiashara, hivyo anatakiwa kutafuta ya michezo ili arejee kuitumikia klabu hiyo.
Alisema nyota huyo alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo, jana alikwenda kwenye Ubalozi wa Uturuki kwa ajili ya kuomba viza ya kimichezo na wakati wowote atakapokamilisha taratibu husika atarejea kukipiga nchini humo.
Na kurejea kwa nyota huyo hakutokani na kuchelewa kwa ITC, kwa kuwa walishamtumia tangu Februari 12, kupitia shirikisho la soka la nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment