tuwasiliane

Saturday, February 18, 2012

18 FEB. MZEE YUSUPH KUREJEA NA VITU VIPYA KUTOKA MAREKANI


Naye Mfalme huyo alisema kwamba mabli na maonesho anayoendelea kuyafanya nchini Marekani, amekuwa akijifunza mengi yahusuyo Muziki.

Huku zikiwa zimebaki siku tatu tu kabla kurejea kutoka nchini Marekani, Kiongozi wa Mabingwa wa Mipasho, Mzee Yussuf 'Mfalme' ametamba kutua nchini akiwa na vionjo vipya vya kila aina kutona nchini Marekani.

Si mwingine bali ni Mfalme Yussuf alisema kwamba kwa kipindi chote cha takribani mwezi mmoja ziarani Marekani, amenasa mbinu nyingi za kimuziki za namna ya kuwaloga wapenzi na mashabiki jukwaani.

Kwani Onyesho lake la kwanza nyumbani litakuwa ni Februari 21, ndani ya Ukumbi wa Ikwete Lodge, Vikindu, Pwani nitakakoanza kuwapa mashabiki vionjo vipya vya Marekani.

Yussuf anayetamba kwa utunzi, uimbaji na upapasaji kinanda, amewaomba mashabiki wa Kinondoni kukaa mkao wa kula, kwani Februari 26, kundi lake litamwaga burudani nzito kwenye ukumbi wa Travertine Hotel hapa Jijini.

No comments:

Post a Comment