tuwasiliane

Wednesday, February 15, 2012

15 FEB.Kila mchezaji Zambia apewa sh. Mil.90/-


SERIKALI ya Zambia imetangaza kumpatia zawadi ya dola za Marekani 59, 000 (zaidi ya sh. Milioni 90 za Tanzania) kila mchezaji wa kikosi chake cha timu ya taifa ya nchi hiyo ‘Chipolopolo’ ambacho mwishoni mwa wiki kilitwaa ubingwa wa Afrika.

"Serikali imewapa kila mmoja dola 59 000, na zawadi hiyo ni mbali na zawadi ambazo kampuni mbalimbali zinaweza kuamua kuwazawadia. Fedha hizo ni kutoka serikalini," Waziri wa Michezo Chishimba Kambwili alisema kwenye radio ya Taifa ya nchi hiyo (ZNBC).

Zambia ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo wa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya kuinyuka kwa mikwaju ya penalti 8-7, baada ya kutoka suluhu kwa muda wa dakika 120 dhidi ya Ivory Coast, ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Fainali hizo zilifanyika kwenye mji mkuu wa Gabon, Libreville, ambao pwani yake ndipo ndege ya jeshi iliyokuwa imebeba kikosi cha wachezaji wa timu ya taifa ya Zambia ilianguka kwenye bahari ya Atlantic mwaka 1993 na kuua wachezaji wote waliokuwemo kwenye ndege hiyo pamoja na wafanyakazi wake.

Ushindi huo wa Zambia ulipokewa kwa shangwe, ambapo mashuja wa michuano hiyo wachezaji wa Chipolopolo walirejea nyumbani Zambia juzi na kupokelewa kishujaa na umati mkubwa wa watu kiasi cha 200,000 ambao ulikusanyika kwenye Uwanja wa Maonyesho wa Lusaka .

Hali ambayo ilisababisha wachezaji hao pamoja na maofisa wa Serikali kuondolewa kiwanjani hapo baada ya mashabiki hao walikuwa na furaha ya kupitiliza kushindwa kufuata utaratibu hali ambayo ilionekana ingesababisha kutokea fujo.

Lakini pamoja na kuwepo furaha kutokana na ushindi huo, pia ulipokewa kwa majonzi kwenye eneo ambalo walizikwa wachezaji wa kikosi wa taifa hilo waliopoteza uhai mwaka 1993, ambako Rais wa Zambia Michael Sata jana alitarajiwa kuweka shada la maua kwa ajili ya kuwaenzi nyota hao ambao waliiletea sifa taifa hilo enzi zao uhai wao.

Mbali na zawadi hiyo iliyotolewa na Serikali, Kampuni ya Bia ya Zambia (B) tayari ilikwishasema itatoa Kwacha milioni 400 kwa ajili ya timu hiyo endapo ingetwaa taji hilo la Afrika , kampuni hiyo ya Bia ya Zambia inaidhamini Chipolopolo kupitia bia yake ya Mosi Larger

No comments:

Post a Comment