tuwasiliane

Wednesday, February 15, 2012

15 FEB. Ajinyonga na kumwachia ujumbe mke wa mtu!


Katika hali isiyotegemewa mkazi mmoja wa Kibamba, aliyefahamika kwa jina la Hamis Tumbuka , amekutwa amejinyonga kwenye mti na kuacha ujumbe uliomtaka msichana anayeitwa Ashura ashuhudie atakavyozikwa.

Tumbuka aliyekuwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani aliacha ujumbe uliosema, “Naomba Waislamu wanizike hapa hapa na Ashura ashuhudie ninavyozikwa..., Ashura nakupenda uishi salama na mumeo.”

No comments:

Post a Comment