RAIS Jakaya Kikwetea ataongoza mamia ya mashabiki wa soka kushuhudia Kombe la UEFA litakapotua nchini Machi 24.
Akizungumza jana, Mkurugenzi wa Maendeleo wa Agape Televisheni ambao ndio wenyeji wa kombe hilo, Steven Mshana alisema mara baada ya kombe hilo kutua nchini litapelekwa viwanja vya Ghymkhana na mashabiki wataongozwa na mkuu huyo wa nchini kulishuhudia.
"Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Tanzania kupata fursa ya kushuhudia makombe makubwa ya soka duniani," alisema Mshana
"Kombe hili litazunguka katika mabara matatu, bara la Asia litaenda China, halafu litaenda Amerika ya Kusini. Afrika linakuja Tanzania na Kenya tu," alisema
Alisema kombe hilo litakaa nchini kwa muda wa siku tatu kabla ya kuelekea Kenya.
"Kwa sasa tunafanya mazungumzo na TFF na Wizara ya Michezo kuangalia utaratibu utakaotumika wakati kombe hilo litakapowasili."
Mshana alisema pia kampuni yake ya Agepe Associate kupitia kituo cha Televisheni cha ATN, ndiyo pekee iliyopewa kibali cha kuonyesha michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
source mwananchi
No comments:
Post a Comment