tuwasiliane

Sunday, February 5, 2012

05 FEB.AZAM YAISHUSHA YANGA



Wagumu toka Arusha JKT Oljoro wamebebeshwa viloba vitatu vya chapa Azam katika uwanja wa Azam hii leo, katika muendelezo wa ligi kuu ya vodacom.

JKT Oljoro kama kawaida yao waliingia uwanjani baada ya wachezaji wa Azam na kuuzunguka uwanja huo hali ambayo imefananishwa na imani za kishirikina, hivyo kuwapelekea wachezaji wa Azam kuwafurugia walipofika katika upande wao.

Ndani ya mchezo Oljoro walikuwa wa mwanzo kuziona nyavu katika dakika ya 12, lakini refa alilikataa baada ya mshika kibendera kunyoosha kibendera kuashilia mfungaji alikuwa kaotea.

Katika dakika 15 za mwanzo mchezo ulibalance na kuanza kuashiria mchezo kumalizika kwa sare, lakini kiungo mwenye timu Salum Abubakari 'Sure Boy' aliuchopu mpira uliomkuta mshambuliaji hatari wa Azam FC, John Bocco na kuunga kwa kichwa murua kabisa na kuandikia Azam goli la kwanza na la 11 msimu huu katika dakika ya 22.

Wakati wakijiuliza nini kimetokea Sure Boy alimgusia Abdi Kasim Babi na akiwa nje ya box Ngassa na Bocco wakifungua pembeni na Babi bila ajizi akamgusia Ngassa na kuandika goli la pili katika dakika ya 26 na kupeleka Azam mapumziko kifua mbele.

Kipindi cha pili kilianza kwa JKT Oljoro kuliandama goli la Azam kwa dakika 10 za mwanzo bila mafanikio, na katika dakika 55 kipa wa Oljoro alimpasia Babi kufuatia presha aliyopata toka kwa John Bocco na bila ajizi Babi alitupia goli la 3, na kuwafanya Azam kuchukua point 3 na goli 3.

Katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera, Kagera Sugar wamekubali kuchapwa goli 1-0 na JKT Ruvu. Goli hilo la JKT Ruvu lilifungwa na Shaydu kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona.

MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Simba SC (16) 34
2. Azam FC (16) 32
3. Yanga (15) 31
4. JKT Oljoro (16) 26
5. Mtibwa Sugar (15) 22
6. Kagera Sugar (16) 20
7. JKT Ruvu (16) 20
8. Ruvu Shooting (16) 18
9. African Lyon (15) 17
10. Coastal Union (16) 17
11. Moro United (16) 15
12. Villa Squad (16) 13
13. Toto Africa (15) 13
14. Polisi Dodoma (16) 13

No comments:

Post a Comment