
Alisema kwamba amevianika hata vitu ambavyo, akiviona anavijutia lakini ameamu kufanya hivyo huku akiamini litakuwa ni somo kwa vijana wadogo wenye umri kama wake.
Si mwingine bali ni yule Mwigizaji anayechipukia kwa spidi mia moja Elizabeth Michael ‘Lulu’, ameamua kuyaanika maisha yake kupitia Filamu yake ya kwanza itwayo ‘Foolish Age’, inayotarajiwa kuingia sokoni siku za usoni kuanzia sasa.
Lulu alisema ndani ya Filamu hiyo pia atatumia jina la Lulu, na kwa kiasi kikubwa itazungumzia sehemu ya maisha yake.
Mbali na hilo alisema kuna vitu vingi amevipata kwenye maisha ya ukweli, ambavyo vitaonekana kwenye hiyo ‘Filamu’.
Alisema kama vile wakati akitoroka nyumbani kwenda disko, na kuwa kwenye makundi yasiyo mazuri.
Katika Filamu hiyo amewashirikisha wasanii mbalimbali wenye majina, miongoni mwao wakiwa Mboto na Hasheem Kambi na kwamba mashabiki wasubiri vitu vyake.
SOURCE DARHOTWIRE
No comments:
Post a Comment