
Hatimae Ivo Mapunda amesaini mkataba na timu kongwe ya Kenya ya Gormahia. Ivo mapunda aliekuwa chaguo namba moja enzi za Maximo, akizichezea kabla timu za Tanzania Prisons, African Lyon, ST George (Ethiopia), Yanga na kabla ya kwenda Gormahia alikuwa Bandari ya Kenya.
Ataanza kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao, na kuna uwezekano mkubwa akawa ni chaguo namba moja.
Taarifa kabla iliandikwa na shabiki wa kutoka Kenya katika ukurasa wa kandanda facebook akisema Ivo mapunda amejiunga na Gormahia. Hapo kabla Miltone Reyes shabiki huyo alionyesha wasiwasi wake wa je kama angejiunga na Leopards ingekuwa vigumu kupata namba ila kama angejiunga na Gormahia kungekuwa na uwezekano wa kupata namba.
“Nimesaini Mkataba na Gormahia FC leo. Namshukuru MUNGU sana, pia nawashukuru wote mlionipa sapoti nilipokuwa na timu ya BANDARI FC, naomba mzidi kuwa nami SITAWAANGUSHA, tuombeane mafanikio,” hii ndio iliyokuwa tarifa katika ukurasa wake wa facebook.
No comments:
Post a Comment