tuwasiliane

Wednesday, December 14, 2011

14 DEC.FRANCIS CHEKA NA KARAMA NYILAWILA ULINGONI JANUARI 28



Wakali hao wa ngumi hawajawahi kutwangana mpambano ambao umewafanya mashabiki kuhisi kwamba, mabondia hao wanaogopana.

Si wengine bali ni ile miamba miwili katika ngumi hapa nchini, Bingwa wa Mabara Francis Cheka (SMG) na bingwa wa Dunia Karama Nyilawila (Kapten) wanatarajia kuchapana hapo Januari 28 mwaka huu.

Naye Promota wa pambano hilo Philemon Kyando 'Don King', alisema kwamba pambano hilo litapigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Lengo la pambano hilo kwa Miamba hiyo Cheka na Nyilawila, ni kuondoa uvumi kwamba mabondia hao wanaogopana lakini ni kuurudisha mchezo wa ngumi kwenye chati yake kama ilivyokuwa hapo awali.

No comments:

Post a Comment