tuwasiliane

Sunday, December 11, 2011

11 DEC.UGANDA BINGWA CECAFA,KILI STARS HOI


Uganda imepata ubingwa wa michuano ya soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Senior Challenge Cup mwaka 2011 baada ya kuifunga timu ya Rwanda katika mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Tanzania.

Uganda imeifunga timu ya Rwanda kwa penalti 3-2 baada ya kumaliza dakika 90 za kawaida zikiwa zimefungana 2-2 ambapo ziliongwezwa dakika 30 ambazo nazo hazikuweza kumpata mshindi.

Kipa wa Uganda Abby Dhaira ndiye aliyedaka penalti ya mwisho ya Rwanda iliyopigwa na Ngabo Albert baada kumaliza ikiwa imepata penalti 3 na kukosa 2.
Rwanda ilipata penalti 2 na kukosa 3.Katika mchezo wa kutafuta nafasi ya tatu, Sudan iliifunga Tanzania bara 1-0.Uganda wamepata kombe pamoja na kitita cha dola za Marekani 30,000, mshindi wa pili, Rwanda amepewa dola 20,000, wakati Sudan imenyakua dola 10,000.

No comments:

Post a Comment