tuwasiliane

Thursday, December 8, 2011

08 DEC. CAF KUWANOA MAKOCHA WA KIBONGO


Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limepitisha majina ya makocha 40 wa Tanzania kushiriki katika kozi ya ukocha ya leseni B ya shirikisho hilo itakayofanyika Dar es Salaam Desemba kuanzia 19-22..

Kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura makocha wote waliopitishwa wana cheti cha ukocha cha ngazi pevu ambapo kozi hiyo awali walikuwa wanapata makocha wowote bila kujali elimu aliyokuwa nayo.

Aliwataja makocha hao ambao wote ni wazoefu wa soka muda mrefu hapa nchini na mikoa wanayotoka kwenye mabano ni pamoja na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Leodegar Tenga, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Kassim Majaliwa (Dar es Salaam) na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera (Morogoro).

Wengine ni Michael Bundala (Dar es Salaam), George Komba (Dodoma), John Simkoko (Morogoro), Juma Mwambusi, Samson Mkisi (Mbeya), Sylvester Marsh (Mwanza),Salum Madadi (Dar es Salaam), Mohamed Nyange (Dodoma), Madaraka Bendera, Ally Mtumwa (Arusha), Charles Mkwasa, Idd Mshangama, Hassan Mlwilo (Dar es Salaam), Mohamed Msomali (Morogoro), Mbarouk Nyenga (Tanga) na Leopard Mukebezi (Dar es Salaam).

"Katika orodha hiyo pia wamo Mohamed Tall , Mshindo Msolla (Dar es Salaam), Abdallah Hussein (Kilimanjaro), Oscar Korosso (Mbeya), Charles Kilinda (Pwani), Fred Minziro (Dar es Salaam), Salum Mayanga (Kagera), Hamimi Mawazo (Mtwara), Rogasian Kaijage (Kagera), Eugene Mwasamaki (Dar es Salaam) na Mohamed Mozi (Tabora),” alisema Wambura.

Pia wamo Charles Matoke (Dar es Salaam), Peter Magomba (Singida), Abdul Mingange (Dar es Salaam), Juma Nsanya (Tabora), Jamhuri Kihwelo (Dar es Salaam), Gilbert Mahinya (Tabora), Juma Mzigila (Morogoro), Joseph Sehaba, Charles Mngodo (Dodoma) na Mohamed Rishard Adolph (Dar es Salaam).

No comments:

Post a Comment