
meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson anaamini kikosi chake kitafuzu hatua ya mtoano ya Ubingwa wa Vilabu vya Ulaya licha ya kutoka sare na Benfica.
Sir Alex Ferguson aonesha matumaini ya kusonga mbele
Sir Alex Ferguson aonesha matumaini ya kusonga mbele
United inahitaji angalao pointi moja watakapokabiliana na Basel katika mechi yao ya mwisho ya kundi C ili ifuzu hatua inayofuata baada ya matokeo ya Jumanne ya sare ya 2-2 na Benfica.
Lakini matumaini ya kuongoza katika kundi lao ni finyu kutokana na Benfica mechi yao ya mwisho watakabililiana na Otelul Galati isiyokuwa na pointi hata moja na imeonekana dhaifu katika kundi lao.
"Utakuwa mchezo mgumu dhidi ya Basel. Lakini nina imani na kikosi changu," alisema Ferguson.
"Benfica lazima watashinda dhidi ya Galati lakini tunahitaji kushinda kwa mbwembwe."
Wakimaliza nafasi ya pili katika kundi lao itakuwa na maana Manchester United huenda mapema wakakabiliana na timu kama Barcelona, Real Madrid, Inter Milan au Bayern Munich katika hatua ya timu 16 za mwisho, lakini Ferguson hana wasiwasi na hilo.
No comments:
Post a Comment