Sunday, May 13, 2012
13 MAY.DIDA ATUA AZAM NA KUFUNGA USAJILI WA AZAM
Mabingwa wa kombe la Mapinduzi na waakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Shirikisho Mwakani na Kombe la Kagame Azam FC wamekamilisha usajili wao wa msimu ujao kwa kuwaongeza kikosi wachezaji wawili ambao ni Kipa wa Mtibwa Sugar Deo Munishi Dida na mshambuliaji toka Randers FC ya Denmark Mkenya George Blackberry Odhiambo.
Deo Munich alisajiliwa Mtibwa Sugar msimu uliokwisha kuziba pengo la Shaban Kado aliyetimkia Yanga, na kipa huyo wazamani wa Manyema na Simba SC ameonyesha kiwango kizuri msimu huu na kulivutia benchi la Azam lililo ondokewa na kipa Mserbia Circovic mapema mwaka huu kwenda Vetnam.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo katika mtandao wa Azam FC(www.azamfc.co.tz) zinaelezea kuwa klabu hiyo itatowa wachezaji wanne kwa mkopo kwenda klabu hiyo, huku majina ya wachezaji hayo kutowekwa bayana.
"Kwa maana hiyo Azam FC imesajili wachezaji 27 na haijaacha mchezaji hata mmoja ingawa mwalimu Stewart Hall ameacha maagizo ya kupelekwa kwa mkopo wachezaji wanne, ambapo wa kiungo katikati ni wawili, kiungo pembeni mmoja na golikipa mmoja ili kuwapa nafasi ya kucheza kutokana na mlundikano wa wachezaji kwenye nafasi hizo," ilieleza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa: "Pia Azam FC inajivunia nyota wake wa Under 20 ambao imewapandisha juu ambao ni Aishi Salum, Juckson Wandwi, Dizana, Ibrahim Rajab Jeba na Joseph Kimwaga."
Kikosi Kamili cha Azam FC msimu ujao:
Magolikipa
Mwadini Ally, Deo Munishi "Dida", Aishi Salum na Jackson Wandwi
Mabeki
Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Samih HajiNuhu, Luckson Kakolaki, Said Moradi, George Owino na Aggrey Morris.
Viungo
Kipre Bolou, Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum Abubakar, AbdiKassim Sadala, Ramadhani Selemani Chombo, Abdulghani Ghulam, Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz Stima, na Ibrahim Joel Mwaipopo.
Washambuliaji
Kipre Tchetche, Mrisho Ngasa, Zahoro Pazi, Khamis Mcha, na George Odhiambo "Blackberry", Gaudence Mwaikimba na mchezaji bora wa Azam FC John Raphael Bocco "Adebayor"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment