Sunday, May 13, 2012
13 MAY. SIMBA VS AL AHLY SHANDY LEO SAA 2 USIKU
SIMBA leo itakuwa uwanjani Sudan kumenyana na Al Ahly Shendi ya huko katika mechi
ya pili ya raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho.
Simba iliondoka jijini Jumanne kuelekea Sudan kwa ajili ya mechi hiyo ambapo hata hivyo hawakupata mapokezi mazuri kutoka kwa wenyeji wao hali ilioufanya uongozi wa klabu
hiyo kuazimia kupeleka malalamiko (CAF).
Simba leo inahitaji ushindi au kama kufungwa isiwe zaidi ya mabao 3-0 ili isonge mbele hatua inayofuata ya michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa wiki mbili zilizopita kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Habari kutoka Sudan zinasema pamoja na vituko walivyofanyiwa na wenyeji, lakini kikosi cha Simba kiko imara kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa katika mji wa Shendi.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga Simba imefanyiwa vitendo ambavyo si vya kiuanamichezo ikiwa ni pamoja na kusafirishwa umbali mrefu, kupewa chakula usiku sana pamoja na kulazwa kwenye hosteli badala ya hoteli nzuri kama walivyofanyiwa wao
walipofika nchini.
Kamwaga alisema wachezaji wako kwenye hali nzuri na kocha Milovan Circovick ameahidi kuibuka na ushindi.
“Kila kitu chetu kwa upande wa benchi la ufundi kiko sawa, pamoja na vurugu zao lakini tunaamini dakika 90 uwanjani ndio zitaongea,” alisema Kamwaga.
“Wachezaji wako kwenye ari kubwa pamoja na mizengwe ya hapa na pale, kwani hawakukatishwa tamaa badala yake walifanya mazoezi wenyewe pamoja na kocha kuwapa
mapumziko… wachezaji wanasema lengo lao ni kuvuka raundi inayofuata na watavuka hata wakiwafanyiwa vituko,”alisema Kamwaga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment