tuwasiliane

Sunday, January 8, 2012

08 JAN. Msamaha wamrudisha Diamond kwa PILATO!


Nyota wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, Jumatatu atapanda kwenye (Pilato) kizimba cha Mahakama ya Wilaya, Iringa akikabiliwa na msala wa kuharibu mali.

Taarifa iliyofika mezani kwetu imedodosa kuwa, msanii huyo anatakiwa kutinga mahakamani hapo asubuhi ya saa 2:30, bila kukosa huku ikisemekana mlalamikaji alilazimika kufungua kesi hiyo kufuatia mlalamikiwa kupuuza makubaliano.

Diamond alishikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Iringa siku moja kabla ya kuingia kwa mwaka mpya wa 2012 akidaiwa kuharibu mali ya mwandishi wa habari, Francis Godwin.

Katika sakata hilo, Diamond alitakiwa kumlipa mwandishi huyo Sh. milioni 1.8, lakini akaomba hadi Sh. milioni 1.7 na kumuomba msahama yaishe.

Hata hivyo, taarifa zilidai kuwa alifanikiwa kulipa kiasi hicho cha fedha, lakini hakuomba msamaha hivyo kesi ‘kufowadiwa’ mahakamani

No comments:

Post a Comment