tuwasiliane

Sunday, January 8, 2012

08 JAN. Diamond kucheza kimataifa zaidi!


zee wa Totoz Naseeb Abdul maarufu kwa jina ‘Diamond platinum baby’, amefunguka kuwa ndani ya mwaka 2012 amejipanga kutoka kimataifa zaidi kwa kuwashirikisha wasanii maarufu kutoka nje ya nchi katika nyimbo zake.

Kwa mujibu wa Diamond, tayari ameshaanza kujipanga juu ya hilo toka mwaka jana na mwaka huu ndio atalitimiza, kwa kuwashirikisha katika nyimbo mbalimbali ambazo atazitoa mwaka huu.

“Huu ni mmoja wa mikakati yangu katika mwaka huu 2012 na nina imani nitafanikiwa juu ya hilo, kwa kuwa nimejipanga na nitafanya hivyo,” alisema Diamond.

Licha ya kuwa na mipango hiyo, Diamond hakuwa tayari kuwaweka wazi wasanii hao wa nje ambao anaazimia kufanya nao kazi.

No comments:

Post a Comment