Sunday, January 8, 2012
08 JAN. ANC yamazila sherehe za kutimiza karne
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amehutubia maelfu ya wafuasi wa ANC, katika sherehe zinazomalizika leo za kuadhimisha miaka 100 tangu chama hicho kuundwa - chama kikongwe kabisa cha ukombozi barani Afrika.
Mauaji ya Sharpeville, Afrika Kusini mwaka wa 1960
Bwana Zuma alisema leo ni siku ya furaha kwa watu wa Afrika Kusini, ambao waliangamiza ukoloni na ubaguzi wa rangi, kwa kusaidiwa na Afrika na ulimwengu.
Bwana Nelson Mandela hakuweza kuhudhuria kwa sababu ni dhaifu.
ANC hivi karibuni imekumbwa na kashfa za rushwa na mizozo ndani ya chama lakini bado kina wafuasi wengi
Kati ya wageni waliohudhuria sherehe hizo ni Kasisi Jesse Jackson, mwanaharakati maarufu wa Marekani wa kutetea haki za weusi.
Alisema: "Baada ya karne moja - kutoka madhalilisho, kachomoza Nelson Mandela, Thabo Mbeki, Jacob Zuma, na Barack Obama.
Ni karne ya mifano ya kuvuka vizingiti vikubwa.
Na khofu waliyokuwa nayo wazungu - kwamba weusi watalipiza kisasi - hayakutokea hayo".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment