Thursday, January 5, 2012
05 JAN.NGOMA MPYA YA JAY MOE NA MIMMS YAVUJA
Ngoma mpya ya Jay Moe na ya kwanza kwa mwaka huu kutoka Bongo Records, iliyotarajiwa kutoka Jumamosi ya wiki hii ya tarehe 7 Jan 2012 inayoitwa 'U CAN NEVER B ME' ikiwa imewashirikisha mkali Mimms kutoka Marekani Immu Cabir kutoka Mozambique na Avid kutoka bongo imeleak (Imevuja).
Akiongelea kuvuja kwa pini hilo mmiliki na producer wa Bongo Records, Pfunk (Majani) amesema ameshtushwa na kuvuja huko kwani na yeye alikuta ametumiwa pini hilo kwenye email yake kama zawadi ya mwaka mpya na tayari limeshasambaa kwa watu wengi sana.
Hata hivyo Pfunk anasema pini hilo halijakamilika kama alivyokuwa anataka na ameomba wapenzi wa muziki wasubiri lenyewe la ukweli atakalorelease tarehe jumamosi hii ya tarehe 7.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment