Saturday, May 12, 2012
12 MAY.TP MAZEMBE WAJIFICHA HOTELINI KUKWEPA VURUGU
TP Mazembe wajificha Hotelini kuogopa vurugu nchini Sudan
Viongozi na wachezaji wa klabu ya TP Mazembe ya Kongo walibakia wamejificha kwenye hoteli waliyofikia nchini Sudan huku polisi wa nchini humo wakiwasisitiza mashabiki wa Mazembe waliombatana na timu kutotoka nje ya hoteli ambazo wamefikia kuepusha vurugu ambazo zinaweza kujitokeza. Hapo jana(Alhamisi) baada ya Mazembe kuwasili kwenye jiji la Khartoum nchini Sudan kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya pili ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Afrika itakayopigwa siku ya jumamosi dhidi ya Al Merreick ya nchini humo kwenye uwanja wa Omdurman Stadium, Kwenye mechi ya awali iliyopigwa Kongo Mazembe waliibuka kidedea kwa ushindi wa goli 2-0.
Katika mapokezi hayo mashabiki wa Al Merreick walianza kufanya vurugu kwa kuwarushia mawe,makopo na kutoa maneno makali ya kuchochea vurugu kwa mashabiki wa Mazembe. Taarifa kutoka kwa kamanda wa polisi wa nchini humo zilisema: “Tunawaomba Viongozi wa TP mazembe na wachezaji kwa ujumla kutotoka na kuenda kutembea mjini pia tunaomba muwashauri na mashabiki wenu kutozurura hovyo mitaani kwa sababu za kiusalama kwani kuna uwezekano wa kutokea vurugu.” Taarifa hiyo ilitolewa na kamanda wa polisi wa nchini humo kwenda kwa mkuu wa msafara wa TP Mazembe Frederic Kitenge.
Ilibidi kocha wa timu hiyo ya Mazembe Lamine N’Diaye ahairishe programu ya mazoezi ambapo awali alipanga timu ifanye mazoezi ya kujiandaa siku ya Alhamisi jioni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment