tuwasiliane

Saturday, May 12, 2012

12 MAY. WAKENYA WAKIUME WAOANA UINGEREZA



Harusi ya kwanza ya wakenya wapenzi wa jinsia moja imefanyika mjini London Uingereza. Ndoa kati ya watu wa jinsia moja hairuhisiwi kwa mujibu wa sheria za Kenya, inaaminika ndiyo sababu watu wakaoana nje ya nchi.

Ni ndoa ya kwanza ya aina hiyo kufanyika hadharani kati ya wanaume wawili wanaotoka Afrika Mashariki, mjini London chini ya sheria iliyopitishwa mwaka 2005 nchini Uingereza ikiruhusu kutambulika kisheria uhusiano kati ya wapenzi wa jinsia moja.

Daniel Chege Gichia mwenye umri wa miaka 39 alimuoa Charles Ngengi mwenye umri wa miaka 40 aliyekuja London mahsusi kwa shughuli hiyo katika ukumbi wa Islington kaskazini mwa London.

Wengi wa wageni wa maharusi hao walikuwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja au wanaotetea ndoa kama hizo pamoja na wale wasiobughudhiwa na uhusiano kama huo.
Wawili hao wanaotoka mkoa wa kati , wilaya ya Murang'a wanajiandaa kwenda Kenya kwa fungate yao baadaye mwezi .kwa namna hiyo unaona ni jinsi gani shetani anavyo udanganya ulimwengu na kuupotosha,hakika haya ni matendo ya kuzimu

No comments:

Post a Comment