MWANAMKE aliyejitambulisha kwa jina la Devotha Ernesta, mkazi wa Msowero wilayani Kilosa amejifungua watoto wa mapacha walioungana kuanzia sehemu ya kichwa mpaka kiwiliwili wakiwa na miguu minne na mikono minne.
Tukio hilo lilitokea Mei 8, mwaka huu kwenye Hospitali ya Wilaya Kilosa baada ya mwanamke huyo kufika hospitalini hapo akiwa na ujauzito uliokamilika siku za kujifungua.
Muda ulipofika ndipo alipojifungua watototo walioungana wakiwa na uzito wa kilo nne lakini muda mchache baada ya kuzaliwa walifariki dunia.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Moses Mwemsanga alisema kuzaliwa kwa watoto hao ni hali ya kawaida inayoweza kutokea kwa mtu yeyote na kwamba kunasababishwa na mbegu za kike na zakiume kuungana na baadye kushindwa kugawanyika.
''Hawa walikuwa watoto mapacha, lakini ilishindikana kugawanyika baada ya mbegu za mwanamke na mwanaume kuungana,ni hali ya kawaida ambayo inaweza kutokea kwa mtu yeyote ingawa hutokea kwa nadra sana''alisema Dk Mwemsanga.
Kwaupande wake, Mwanamke aliyejifungua watoto hao, Devotha Ernest alisema katika maisha yake hakuwai kuona mtoto kama huyo aliyejifungua yeye na hawezi kuhusisha na imani za kishirikina bali ni mapenzi ya mungu.
''Nilikuwa natamani sana nijifungue salama nipate furaha na mwanangu lakini mwenyezi Mungu ameamua kutekeleza alichokusudia kwa mapenzi yake na siwezi kuhusisha na tukio la kishirikina kutokana na kujifungua mtoto huyu bali na mapenzi yake mungu.
Kufuatia kuzaliwa kwa watoto hao wananchi wa Mji wa Kilosa na vitongoji vyake walimiminika kwenda kumuangalia mtoto huyo aliyefariki muda mchache baada ya kujifungua na walitoa maoni mbalimbali
No comments:
Post a Comment